Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, salamu za rambirambi kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:
Bismillāhir-Raḥmānir-Raḥīm
(إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَیْهِ رَاجِعُونَ)
Sisi, wanachama wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Bangladesh, kwa masikitiko makubwa, tumepokea taarifa ya jinai nyingine ya waziwazi iliyojaa uovu kutoka kwa utawala dhalimu na batili wa Kizayuni, ambao kwa dharau kubwa na kwa kuzikanyaga sheria na kanuni zote za kimataifa, umetenda jinai ya mashambulizi ya kijeshi ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mashambulizi ambayo yamesababisha kuuawa kishahidi kwa kundi la makamanda waandamizi, wanasayansi wenye maarifa ya juu, pamoja na raia wasio na ulinzi. Tukio hili chungu limeumiza kwa kiasi kikubwa nyoyo za Waislamu wa Bangladesh, hususan waumini wa madhehebu ya Shia.
Baraza hili la Maulamaa, kwa niaba ya Waislamu wote na hasa Mashia wa Bangladesh, linapinga vikali tendo hili la kinyama na ukiukaji wazi wa sheria za kimataifa, na linatoa salamu za rambirambi kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kwa taifa tukufu la Iran.
Tunamuomba Mwenyezimungu Mwingi wa Rehema awainue daraja Mashahidi wa tukio hili, na kuzitunuku subira na uthabiti familia zao zilizofikwa na msiba huu mkubwa.
Tunatumaini kuwa kwa umoja na subira ya mataifa ya Kiislamu, siku si nyingi tutashuhudia kutokomezwa kwa utawala huu batili na mchafu kutoka katika uso wa dunia.
Wassalāmu ʿalaykum warahmatullah
Maoni yako